MASWALI YA MARUDIO YA TAMTHILIA: BEMBEA YA MAISHA
Na Timothy M. Arege
"Kumbuka Mrina haogopi nyuki. Marehemu mamangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishi mwanadamu wala hazipotei bure humalizwa tu na mabuu…. Usifanye hofu. Nikujuavyo mimi hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa ncha yote yanakikomo eti ipo siku haya yote yatapita. Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safi kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na Mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyoeka.
Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi za kutisha."
(a) Bainisha toni mbili katika dondoo hili Alama 2
(b) Eleza sifa za msemaji Alama 6
(c) Eleza umuhimu wa mandhari ya hospitalini Alama 7
"Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi za kutisha."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake Alama 4
(b) Jadili umuhimu wa msemaji katika kujenga tamthilia Bembea ya Maisha Alama 4
(c) Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigwa mstari ukirejelea Bembea ya Maisha kwa hoja kumi na mbili Alama 12
"Eti hajakosa adabu? Mtu ana ubaguzi kama nini! Ana moyo mgumu kama jiwe. Amejaliwa lakini bahili kama mchanga wa dhahabu. Hajui mali ya bahili huliwa na wadudu?"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Tathmini umuhimu wa maswali balagha katika dondoo hili. Alama 2
(c) Toa mifano ya vipengele vingine viwili vya kimtindo katika dondoo hili. Alama 4
(d) Fafanua nafasi ya anayeitwa bahili katika dondoo hili kwa kuijenga tamthilia ya Bembea ya Maisha Alama 10
Kila binanadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake.
(a) Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya maisha. Alama 10
(b) Huku ukitoa mifano mwafaka, kutoka katika tamthilia ya bembea ya maisha, onyesha jinsi mbinu rejeshi ilivyojitokeza. Alama 10
Maji yangekuwa yamewafika shingo basi wangeshindwa kuishi pamoja, Ndoa ni bembea, kuna wakati itakuwa juu na wakati itakuwa chini. Hizo juu-chini chini-juu ndizo utamu wake. Ni kama maisha kwa jumla. Yana pandashuka ndiyo lakini pandashuka hizo ndizo hutupa kuridhika hatimaye tunapozishinda. Maisha yangekuwaje bila hali kubadilika?
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Tambua mbinu nne za kimtindo katika dondoo hili. Alama 4
(c) Kwa kurejelea tamthilia nzima fafanua pandashuka walizopitia wahusika mbalimbali. Alama 7
(d) Kwa hoja tano, jadili umuhimu wa mbinu rejeshi kama ilivyotumiwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 5
"Awali niliona kama mchezo, kumbe ilikuwa kweli! Kauli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silesi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. Siku hazigandi wala jana haitarudi. Sasa jana imebaki kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika."
(a) Fafanua mbinu nne za kutambua sifa za msemaji wa maneno haya. Alama 4
(b) Bainisha toni katika dondoo hili. Alama 2
(c) Changanua mtindo katika dondoo hili. Alama 4
(d) Fafanua umuhimu wa mandhari katika dondoo hili. Alama 6
(e) Eleza maudhui yanayojitokeza katika dondoo hili. Alama 4
"Mgala muuwe na haki umpe."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Tambua mbinu ya kimtindo katika dondoo hili. Alama 1
(c) Eleza umuhimu wa mbinu ya kimtindo uliyotaja hapo juu. Alama 2
(d) Dhibitisha ukweli wa msemaji kwa mujibu wa dondoo Alama 3
(e) "Mila na desturi zetu zimewajenga hivyo walivyo na sisi hivi tulivyo." Imani na itikadi huthaminiwa sana na jamii zetu. Jadili ukweli wa kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya Bembea ya maisha. Alama 10
"...marehemu mamangu alizoea kutuambia kuwa nguvu hazimwishii mwanadamu wala hazipotei bure, humalizwa tu na mabuu. Mwanangu usifanye hofu. Nikujuavyo mimi, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilo na ncha. Yote yana kikomo eti! Ipo siku haya yote yatapita. Mkulima hodari libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safi kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka"
(a) Fafanua vipengele sita vya kimtindo vinavyopatikana kwenye dondoo. Alama 6
(b) Bainisha toni katika dondoo hili. Alama 2
(c) Fafanua umuhimu wa "mwanangu" katika kujenga tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 6
(d) Jadili changamoto sita anazopitia "mwanangu" maishani. Alama 6
(a) "...haikuwa mara moja mnavyofikiria, ilianza pale chuoni. Wenzangu walinipa mvinyo kunirai ulevi."
i. Eleza maudhui matatu yanayojitokeza kwenye dondoo hili. Alama 3
ii. Eleza athari zilizomkumba mhusika anayerejelewa kwa kujitosa katika suala linalodokezwa kwenye dondoo. Alama 7
(b). Eleza jinsi maudhui ya ndoa yalivyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 10
"Huku ndiko kuvumilia hasa. Tazama faraja ilivyoalika sasa"
(a) Weka dondoo hili katika muktadha. Alama 4
(b) Eleza sifa za msemaji katika dondoo. Alama 6
(c) Onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa kwa kurejelea tamthilia ya: Bembea ya Maisha. Alama 10
Maskini mke wangu! Kumbe ugonjwa haukumsaza mwaka baada ya mwaka. Umemla bila huruma. Awali niliona kama mchezo. Kumbe ilikuwa kweli! Kauli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silesi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. (Kimya). Siku hazigandiwala jana hairudi. Sasa jana imebaki kuwa kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika. (Kimya). Kwa bahati nzuri bado tupo. Ninaweza kuiachia dunia tabasamu iwe silesi kwa vizazi vijavyo na kila mwenye nia njema. (Kimya). Siwezi kuendelea kuishi hivi. Sasa nimekata shauri. Lazima niache njia ya zamani na kuifuata mpya. Maisha mapya. Pombe! (kama anayeisemea pombe). Umenichezesha kama mwanasesere kwa muda mrefu. Umeninyima fursa ya kuielewa familia yangu. Hapana! Siku zangu za uzeeni lazima nizitumie kumwangalia mke wangu mgonjwa. Lazima nimshukuru kwa vitendo kwa jinsi alivyojitolea kuijenga familia yetu. (anapunga mkono.) Kwaheri pombe. Buriani.
ii. Bainisha toni ya dondoo hili. Alama 2
iii) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kuijenga tamthilia nzima. Alama 8
"Ndiyo inifae nini? Mimi mwenyewe sikuwa mnyonge. Ninajua maana ya bidii. Lakini vilevile ninajua kuwa bidii pekee haifaulishi kila jambo."
i. Eleza muktadha wa dondoo. Alama 4
ii. Eleza sifa nne za msemewa. Alama 4
(b) "Wala hakuna wapatanao kama sahani na kawa." Kauli hii inadokeza kuwa migororo lazima iwepo katika jamii. Fafanua migogoro iliyojitokeza kwenye Tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 12
"Sisi tuna bahati ya mtende mtoto kutusikiliza na kutupiga jeki."
(a) Tambua muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Kwa kutoa mifano minne, eleza vipi mrejelewa amewapiga jeki. Alama 4
(c) Taja na ufafanue mbinu iliyojitokeza katika dondoo. Alama 2
(d) Fafanua sifa sita za mnenewa. Alama 6
(e) Tambua na ufafanue maudhui yoyote mawili yanayojitokeza katika dondoo. Alama 4
(a) Kwa kurejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha, eleza namna mwanamke alivyosawiriwa. Alama 10
(c) Angazia kwa mifano mwafaka namna ambavyo maudhui ya utu yanavyojitokeza katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 10
Mungu alipoyajibu maombi yangu na kunifungulia milango ya heri, mliufanya uso wangu kung'aa kwa furaha. Nilijihisi kama mtu aliyeingia katika likizo ya afueni.
(a) Eleza muktadha wa maneno haya. Alama 4
(b) Bainisha toni inayojitokeza katika dondoo. Alama 1
(c) Eleza aina tatu za taswira zinazojitokeza katika dondoo. Alama 3
(d) Jadili umuhimu wa mbinurejeshi kama inavyodhihirika katika tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 12
Wewe sema yako na ya kuazima lakini hiki kidevu changu kwa hilo simo mimi.Mshahara wako sikuombi.Utakavyoupangia ni hiari yako. Nimekununulia gari jipya kabisa. Shughuli utakazolipangia ni maamuzi yako. Wewe si kama wale wanawake ambao hawana kazi wala bazi. Tangu hapo nimekupa ikibali kuiinua familia yako kwa huo mshahara wako. Sijateta wala kununa. Majukumu unayofaa kuyatekeleza nimejitwika mimi ili uweze kuziba nyufa. Kwa bahati nzuri wewe una kazi. Unaweza kuelewa changamoto za mishahara. Mimi ninaelewa kuwa licha ya kitita cha pesa unacholipwa mwisho wa mwezi, bado unajikuta mhitaji maana majukumu ni mengi. Kumbuka nilikuachia mshahara huo ukamsomeshea Asna mpaka ana digrii yake ingawa bahati ya ajira haijamfungulia milango.Salome naye nimemlipia karo shule ya upili na chuoni. Kwa bahati nzuri masomo yamemwitika akapita vizuri na hiyo first class. Ameishi nasi hapa akisoma hadi pale alipobahatika kupata ufadhili wa kwenda kuendeleza masomo yake ng'ambo. Katika hayo yote mimi ninajitahidi kukuelewa. Ingekuwa furaha iliyoje kama mimi vilevile ungenielewa!
(a) Changanua mbinu zozote sita za sanaa katika kifungu hiki. Alama 6
(b) Eleza jinsi maudhui ya uwajibikaji yavyojitokeza katika kifungu. Alama 9
(c) Eleza umuhimu wa Salome. Alama 5
"Huku ndiko kuvumilia hasa. Tazama faraja ilivyoalika sasa"
(a) Weka dondoo hili katika muktadha. Alama 4
(b) Eleza sifa za msemaji katika dondoo. Alama 6
(c) Onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa kwa kurejelea tamthilia ya: Bembea ya Maisha. Alama 10
"Hayo ni ya kale ... na ya kale hayanuki. Wengi hawafuati tena mila hizo. Walimwengu sasa wanavaa sare moja."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Fafanua tamathali mbili za usemi zilizotumika katika dondoo hili. Alama 2
(c) Eleza sifa za mzungumzaji wa kauli hii. Alama 5
(d) Jadili maudhui ya utamaduni kama yanavyojitokeza katika. Tamthilia nzima. Alama 9
"...Hebu fikiri! umepata ajali mbaya. Inakuacha mahututi. Anapita mtu katika gari lake. Kwa Imani anaguswa. Anakufanyia mpango wa Flying Doctors, ndege inafika inakupeleka hospitali. Mwenyewe huyo anakulipia kila kitu! Mtu huyo atakosaje kuwa zawadi kwako?"
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Tambua umuhimu wa mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili. Alama 4
(c) Eleza umuhimu wa anayerejelewa katika dondoo hili. Alama 4
(d) Kwa kutoa hoja zozote nane kutoka kwa tamthilia nzima. Eleza ukweli wa kauli, 'mtu huyo atakosaje kuwa zawadi kwako?' Alama 8
Maskini mke wangu! Kumbe ugonjwa haukumsaza mwaka baada ya mwaka. Umemla bila huruma. Awali niliona kama mchezo. Kumbe ilikuwa kweli! Kauli yake ninaona imesimama. Ni mwele hakika. Laiti ningejua, jana ningeishi tofauti. Silesi zetu za maisha tungezila zilivyokuja kwa furaha. (Kimya). Siku hazigandi wala jana haitarudi. Sasa jana imebaki kuwa kumbukizi baada ya kusombwa na wakati mfano wa mafuriko msimu wa masika. (Kimya). Kwa bahati nzuri bado tupo. Ninaweza kuiachia dunia tabasamu iwe silesi kwa vizazi vijavyo na kila mwenye nia njema. (Kimya). Siwezi kuendelea kuishi hivi. Sasa nimekata shauri. Lazima niache njia ya zamani na kuifuata mpya. Maisha mapya. Pombe! (kama anayesemea pombe). Umenichezesha kama mwanasesere kwa muda mrefu. Umeninyima fursa ya kuielewa familia yangu.
(b) Kauli iliyokolezwa wino katika dondoo inadokeza nia ya kubadilika kwa mzungumzaji. Kwa kurejelea tamthilia nzima, onyesha jinsi mwandishi alivyoshughulikia suala la mabadiliko. Alama 12
"Huku ndiko kuvumilia hasa. Tazama faraja ilivyoalika sasa"
(a) Weka dondoo hili katika muktadha. Alama 4
(b) Eleza sifa za msemaji katika dondoo. Alama 6
(c) Onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa kwa kurejelea tamthilia ya: Bembea ya Maisha Alama 10
...lakini ndio tabia yenu wanawake. Miaka inaposonga kama hivi mnatuona kama... kama... kama...
kama vile tambara bovu.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Eleza umuhimu wa msemewa katika kukuza maudhui. Alama 4
'Lakini watafanyaje? Wakae tu vijijini kwa sababu mji unaenda mbio? Labda bembea yao ya maisha ipo pale mjini!'
(a) Eleza mkutadha wa nukuu Alama 4
(b) Pambanua mtindo katika nukuu Alama 5
(c) Fafanua maudhui ya usasa jinsi yanavyojadiliwa na wahusika katika onyesho husika. Alama 11
(a) Kwa kutoa hoja nane kutoka kwa Tamthilia eleza ni vipi utamaduni ulivyothaminiwa katika jamii hii ya Bembea ya Maisha. Alama 16
(b) Onyesha jinsi faraja ilivyoalika katika maisha ya msemewa kwa kurejelea tamthilia ya: Bembea ya Maisha. Alama 4
"Wakati Mwingine maisha haya hukufanya kujisikia kama abiria kwenye gari liendalo kwa kasi."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Eleza sifa sita za mzungumzaji wa maneno haya. Alama 6
(c) Eleza umuhimu wa mbinu nne iliyotumiwa kwenye dondoo hili. Alama 4
(d) Kwa kurejelea tamthilia, onyesha namna matamanio ya wahusika binafsi yanatikisa mahusiano yao na wahusika wengine. Alama 6
"Sasa mimi ninataka uhuru wangu na sitaki kupigwa kichapo cha mbwa mara kwa mara mpaka nipate ugonjwa wa moyo. Matokeo yake ni haya. Kuna raha gani kama maisha ni kugeuzwa ngoma ukapigwa kwa fujo yote mpaka ukapasuka?"
a. Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
b. Bainisha vipengele vinne vya kimtindo kwenye dondoo hili. Alama 4
c. Kwa kutoa hoja sita, eleza namna asasi ya ndoa inakumbwa na changamoto tele. Alama 6
d. Maisha ya zamani yanatofautiana sana na ya sasa. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 6
Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi ya kutisha. Maisha yetu ni mfano wa mbegu iliyopandwa. Mbegu hiyo haina budi kuoza kwanza ndipo ioteshe mche upendezao. Mche huo wa asili ya mbegu iliyooza, hatimaye hutoa zao la mbegu nyingi ajabu. Ukitazama vizuri, mbegu ile haifi bali huchukua mkondo mwingine wa Maisha.Huchukua umbo jipya lipendelezalo hasa ikiwa itakuwa imeangukia ardhi nzuri.Hapa kijijini japo yapo mawili matatu ya kusinya, ardhi yake si mbaya.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Fafanua ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kurejelea hoja kumi kwenye tamthilia nzima. Alama 10
(c) Bainisha mbinu za kimtindo zinazojitokeza katika kifungu hiki. Alama 6
Jadili namna maudhui ya usaliti yanavyojitokeza katika tamthilia bembea ya Maisha. Alama 20
"Eti hajakosa adabu? Mtu ana ubaguzi kama nini! Ana moyo mgumu kama jiwe! Amejaliwa lakini bahili kama mchanga wa dhahabu. Hajui mali ya bahili huliwa na wadudu?''
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili Alama 4
(b) Tathmini umuhimu wa maswali ya balagha katika dondoo hili Alama 2
(c) Bainisha na kutoa mifano ya vipengele viwili vya kimtindo katika dondoo hili Alama 4
(d) Fafanua umuhimu wa msemewa katika kujenga; Alama 2
i. Wahusika Alama 2
ii. Maudhui Alama 2
(e) Thibitisha kinyume cha kauli iliyopigiwa mstari Alama 6
"Ulinipata mahututi kweli. Ilikuwa ajali mbaya. Zilipotea roho nyingi. Manusura tulikuwa watano tu. Bila msaada wako wa kuita Flying doctors hii leo ningekuwa nimesalia kwenye kumbukumbu tu. Mwezi mzima nilikuwa sijifahamu hospitalini. Japo hukunijua uliguswa ukaipigania nafasi yaku ya kuishi. Sijasahau. Daima nitashukuru kwa wema huu usio wa kawaida. Haikuwa rahisi. Niliponea tundu la sindano..."
(a) Changanua mtindo katika dondoo hili. Alama 8
(b) Onyesha jinsi dhuluma inavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea ya maisha Alama 12
(Maswali yote 52 yamejumuishwa kikamilifu katika toleo hili la HTML)
"...haikuwa mara moja mnavyofikiria. Ilianza pale chuoni. Wenzangu walinipa mvinyo kunirai kuonja ulevi."
(a) Eleza maudhui manne yanayojidokeza katika dondoo hili. Alama 4
(b) Eleza athari za mhusika anayerejelewa kujitosa katika suala linalooredheshwa kwenye dondoo. Alama 6
(c) Kwa kurejelewa mifano tano katika tamthilia ya Bembea ya maisha, eleza tofauti iliopo katika maisha ya ndoa ya zamani na sasa Alama 10
Jadili sababu kumi zilizompeleka mwandishi T. Arege kuandika Tamthilia hii. Alama 20
Si neno mama! (Kimya.) Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi za kutisha.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Bainisha mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili. Alama 4
(c) Fafanua sifa za msemaji. Alama 6
(d) Eleza umuhimu wa mandhari ya dondoo hili. Alama 6
"Bila yeye chombo kingezama. Ni kwamba siwezi kumwambia haya maana atajishaua."
(a) Kwa kutumia hoja tano, fafanua umuhimu wa mnenaji wa kauli hii katika kujenga tamthilia ya "Bembea ya Maisha" Alama 5
(b) Fafanua madhara ya taasubi ya kiume katika jamii kwa mujibu wa tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 7
(c) Kwa kutumia hoja nane, tathmini ukweli wa kauli iliyopigiwa mstari kwa kuzingatia mrejelewa na watu wa jinsia yake. Alama 8
Sara: Mimi ninashukuru kwa hawa alionipa mungu. Nikitaka zaidi nitakuwa mchache wa shukrani.(kimya) Dina nimesemwa sanana kutukanwa kwa sababu ya hawa wasichana wangu. Wewe unajua yote yaliyosemwa, hadharani na faraghani. Si makanisani, si magengeni. Leo nikiviona vitoto hivi vilivyochekwa na kusimangwa jana, vikijiendeshea mambo yao, ninaridhika moyoni. Hata nikiitwa nitaondoka nikiwa nimeridhika. (Anatokwa na machozi) Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha.
i. Changanua maudhui katika dondoo hili alama 3
ii. Bainisha toni katika dondoo hili alama 2
iii. Tambua mbinu tatu za lugha ambazo zimetumiwa katika dondoo hili. alama 3
(b) Jadili jinsi suala la utu linavyoshughulikiwa katika tamthilia ya Bembea Ya Maisha. alama 12
Kila binadamu hukabiliana na mabadiliko katika maisha yake. Jadili kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. alama 20
(a) Eleza namna wahusika mbalimbali wanakabiliana na changamoto zinazowakumba katika tamthilia ya Bembea ya Maisha Alama10
(b) Eleza umuhimu wa mazungumzo kati ya Yona na Neema Alama10
"Miaka inaposonga mnatuona...kama... kama vile tambara bovu. Tambara lisilomjia hata mpiga deki akilini."
(a) Weka dondoo hili katika mkutadha wake. Alama 4
(b) Tambua aina ya taswira katika dondoo hili Alama 2
(c) Eleza umuhimu wa msemaji wa maneno haya katika kujenga Tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 4
(d) Msemanji wa maneno haya na wa jinsia yake wanasawariwa kama tambara bovu.Thibitisha. Alama 10
"Mwanangu usifanye hofu. Nikujuavyo, hukuingia katika bahari si yako. Wala hakuna refu lisilokuwa na ncha. Yote yana kikomo eti! Ipo siku haya yote yatapita. Mkulima hodari ni libasi yake huwa imechakaa na kuchoka lakini moyoni anabaki safi kama theluji kwa kutosheka na tija ya sulubu zake. Huwezi kumlinganisha na mkulima wa nguo safi zilizopigwa pasi zikanyooka."
(b) Jadili changamoto alizopitia msemewa wa maneno haya. Alama 12
(a) Eleza namna wahusika mbalimbali wanakabiliana na changamoto zinazowakumba katika tamthilia ya Bembea ya Maisha Alama10
(b) Eleza umuhimu wa mazungumzo kati ya Yona na Neema Alama10
(c) Matatizo anuwai yanakabili jamii ya Bembea ya Maisha. Eleza kwa kutoa mifano mwafaka. Alama 2
"Tena mtu asiyekujua wala hajapata kukutia jicho! Mpita njia na shughuli zake si ni malaika huyo? Kana kwamba umalaika una ngazi ........"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili. Alama 4
(b) Eleza 'umalaika' wa mrejelewa. Alama 8
(c) Tambua mbinu yoyote ya lugha inayojitokeza katika dondoo hili Alama 4
(d) Fafanua sifa za msemaji. Alama 4
"Lakini ndivyo tabia yenu wanawake. Miaka inaposonga kama hivi mnatuona kama...... kama......kama vile tambara bovu.
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili. alama 4
(b) Bainisha mbinu mbili za kimtindo katika dondoo hili alama 2
(c) Tambua toni ya msemaji katika dondoo hili alama 2
(d) Eleza umuhimu wa msemaji wa dondoo hili. alama 5
(e) Thibitisha ukweli wa kauli iliyopigwa mstari katika dondoo hili. alama 7
(a) Eleza changamoto zinazokumba asasi ya ndoa kwa kurejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. alama 8
(c) Mwandishi wa tamthilia ya Bembea ya Maisha amewajenga wanaume kwa njia hasi na chanya. Jadili. alama 12
" Hivi ndivyo walivyofanya wazee wetu. Mavuno ya kwanza huonjwa na wazee na kutoa baraka"
(a) Fafanua muktadha wa dondoo hili alama. 4
(b) Fafanua umuhimu wa mandhari ya dondoo hili alama. 8
(c) Kwa kurejelea Tamthilia, fafanua changamoto zinazowakumba wakazi wa mijini alama. 8
" Maisha ya sasa hayana fundi. Yanamwendesha kila mtu kama tawi linalosukumwa hadi likang'oka kutoka tagaani na kupeperushwa na upepo. Tukisema ni umri, tutakuwa tunausingizia. Ulimwengu wa sasa haubagui. Wadogo kwa wakubwa, matajiri kwa maskini, wazee kwa vijana, waajiri kwa waajiriwa, wenye ajira na wasiokuwa nayo, wote ukizisikia sauti zao, ni sauti za kilio. ... vipi leo? Mbona kimya?"
(a) Changanua mtindo katika dondoo hili Alama 5
(b) Fafanua jinsi msemaji wa maneno haya anavyojenga maudhui mbali mbali katika tamthilia Alama 7
(c) Kwa kurejelea Tamthilia ya Bembea ya maisha, fafanua namna maisha ya sasa yanamwendesha kila mtu kama tawi Alama. 8
"...wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Hata kijijini wanaishi watu. Watu hao hawakumbwi na dhiki kiasi hiki. Ya nini kung'ang'ania kuyatafuta maisha kama kwamba hayapiti? Maisha ni mshumaa uso mkesha! Ukijiacha sana peupe hata upepo unaweza kuuzima kabla ya kulika hadi nchani."
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili Alama 4
(b) Bainisha toni katika kauli hii Alama 1
(c) Tambua vipengele vitatu vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe Alama 3
(d) Eleza umuhimu wa msemaji katika kuendeleza ploti ya tamthilia hii Alama 12
Mimi nitafuatana nayo pachapacha sawa na mbwa na msasi . Mpaka tuliangushe windo.
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake Alama 4
(b) Bainisha mbinu ya kimtindo uliyotumika katika dondoo hili Alama 2
(c) Huku ukitoa mifano, fafanua sifa sita za msemaji Alama 6
(d) Kwa mujibu wa tamthilia Bembea ya Maisha, ni kwa namna gani vijana walivyosawiriwa katika jamii Alama 8
Mwanamke ana nafasi kubwa katika jamii ya kisasa. Fafanua kauli hii ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 20
"... Hakuna kizuri kijacho kwa urahisi. Mazuri hutoka mbali na wakati mwingine yana hadithi za kutisha."
(a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. Alama 4
(b) Jadili umuhimu wa msemaji katika kujenga tamthilia Bembea ya Maisha. Alama 4
(c) Thibitisha ukweli wa kauli iliyokolezwa ukirejelea tamthilia Bembea ya Maisha kwa hoja kumi na mbili. Alama 12
"Sikiliza basi! Zamani mila zetu hazikuruhusu Watoto wa kike kuenda skuli au kurithi kitu. Sasa wanakwenda na kurithi. Zamani Watoto wa kike walikuwa wanategemea mifuko ya waume zao. Sasa hali ni tofauti. Utamaduni, mil ana desturi zetu zinazidi kuyakubali mabadiliko. Thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake kupanuka. Kuyapuuza haya yote ni kazi bure.
(a) Tambua toni inayojitokeza katika dondoo hili. Alama 2
(b) Bainisha umuhimu wa tamathali mbili za usemi zinazojitokeza katika dondoo hili. Alama 4
(c) Fafanua aina nne za taswira zinazodhihirika katika dondoo hili. Alama 4
(d) Thibitisha ukweli wa kauli kauli iliyopigiwa mstari huku ukirejelea tamthilia ya Bembea ya Maisha. Alama 10
"Maradhi! Madhila yake hayasemeki. Yakimla mtu humthakilisha. Humwacha hoi, hana mbele wala nyuma."
(b) Eleza muktadha wa dondoo hili Alama 4
(c) Fafanua toni katika dondoo hili Alama 1
(d) Eleza sifa nne za msemaji Alama 4
(e) Taja na ufafanue mbinu za kimtindo katika dondoo hili Alama 3
(f) Changanua mtindo Alama 8
"Bunju ni mmoja wenu. Nyote ni wanangu." Hayo ni maneno ya mama. Wakati huo sikuona. Sasa naona. Wanasema mwenye macho haambiwi tazama. Kweli iliyoje! Japo hutokea wakati tukalalamika,ninafikiri Bunju ni zawadi nzuri kwetu. Leo tungekuwa wapi bila Bunju? Maji yangezidi unga. Usingepikika,usingelika.(kimya) Hebu fikiri! Umepata ajali mbaya. Inakuacha mahututi. Anapita mtu katika gari lake. Kwa imani anaguswa. Anakufanyia mpango wa Flying Doctors;ndege inafika na kukupeleka hospitali. Mwenyewe huyo analipia kila kitu!mtu huyo atakosaje kuwa zawadi kwako?
"Mama sijaona baba akipika hivi karibuni."
Kwa kurejelea nukuu hii fafanua usasa na utamaduni vilivyosawiriwa katika tamthilia ya Bembea ya Maisha Alama 20
